Rais Obama ametoa wito kwa
serikali ya Pakistan kuchunguza mtandao ambao ulimpa hifadhi Osama bin
Laden kwenye nyumba ya siri, ambako aliuliwa juma lilopita na makamando
wa Marekani.
Akihojiwa kwenye televisheni, Bwana Obama
alisema hana ushahidi kuonesha kuwa watu ndani ya serikali ya Pakistan
wakimsaidia bin Laden, lakini ni jambo ambalo linafaa kuchunguzwa.
Lakini alisema, lazima kulikuwa na watu wakimsaidia na inafaa kuchunguzwa.
Pakistan imekanusha tuhuma kuwa, kusudi, ilimpa
hifadhi kiongozi wa Al Qaeda, na imetoa amri kufanywe uchunguzi, kwanini
idara yake ya ujasusi ilishindwa kumpata.
No comments:
Post a Comment