Thursday, May 26, 2011

Mali ya Gaddafi yafichuliwa.


Rais Gadaffi
Rais Gadaffi
Imefichuka eneo kulikofichwa mamilioni ya dola mali ya serikali ya Libya.
Hii ni baada ya kufichuliwa kwa stakabadhi ya mamlaka ya uwekezaji nchini humo.

Stakabadhi maalum ya mamlaka ya uwekezaji nchini Libya, ambayo imeonekana na shirika la kutetea haki za binadamu Global Witness, imeonyesha kwamba hapo mwishoni mwa mwezi Juni mwaka jana takriban dola milioni 293 fedha za umma zilihifadhiwa kwenye akaunti za matawi tofauti ya benki ya HSBC ya Uingereza, huku nyingine milioni 275 zikiwekwa kwenye akaunti ya hazina maalum ya benki hiyo.
Kiasi kingine cha dola milioni 110 zimewekwa kwenye akaunti za benki ya Royal Bank Of Scotland huku nayo benki ya Goldmans Sachs ikihifadhi dola milioni 182.
Makao Makuu wa Benki ya Goldmans Sachs
Makao Makuu wa Benki ya Goldmans Sachs
Benki ya Ufaransa Societe General ilipokea dola bilioni 1.8 kutoka kwa mamlaka ya uwekezaji ya Libya, huku nayo benki ya Nomura ya Japan ikiweka kwenye hifadhi yake dola nusu bilioni mali ya serikali ya Libya.
Mali yote hiyo imepigwa tanji baada ya Jumuiya ya Ulaya na Umoja wa Mataifa kutoka amri hiyo.
Wizara ya fedha ya Uingereza imesema hatua hiyo ilichukuliwa kwa sababu kanali Muammar Gaddafi pamoja na jamaa wa familia yake wanathibiti kwa kiwango kikubwa taasisi kuu za kifedha nchini Libya.
Licha ya hayo benki hizo zote zilikaa kimya bila kutoa taarifa hizo kwa umma zikidai kulinda hadhi ya wateja wake.
Hata hivyo shirika la kutetea haki za binadamu Global Witness limesema fedha hizo ni mali ya raia wa Libya na kwamba ipo haja benki hizo kudhibitisha ikiwa zinaendelea kuhifadhi mali hiyo.

No comments: