MAANA YA WOKOVU
“Kwasababu ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako yakuwa Mungu alimfufua katika wafu, UTAOKOKA. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa mtu hukiri hata KUPATA WOKOVU”. (Rum 10:9-10.)
Baada ya kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wako, ni muhimu sana kupata mafundisho ya awali, yatakayokusaidia kujua kwa hakika, maana ya KUOKOKA au WOKOVU; “ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.” (Efe 4:14)
Ndio maana Yesu alisema, tukishawahubiri na kuwasaidia kuokoka, tuwafundishe yote!“Yesu akaja kwao akasema nao, akawaambia, nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na mkiwafundisha kuyashika yale yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote hadi ukamilifu wa dahari”. (Math 28:18-20).
“Basi kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye; wenye shina na wenye kujengwa katika yeye; mmefanywa imara katika imani, kama mlivyofundishwa; mkizidi kutoa shukrani”. (Kol 2:6-7)
“Wakawa wakidumu katika fundisho la Mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali” (Mdo 2:42)
“Muwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu, lakini kwa upole na kwa hofu” (1Pet 3:15)
Watu wengi wamechanganya sana maana halisi ya neno “kuokoka”. Unaweza kupewa tafsiri nyingi na watu, juu ya neno “kuokoka”. Wengine hudhani kuokoka ni dini au dhehebu Fulani la “walokole”. Wengi hudhani wokovu ni maisha Fulani ya kujinyima raha na kujitenga na jamii. Wengi hudhani wokovu ni maisha duni nay a umasikini au kutokuwa na mali za kifahari. Ndani ya fikra za watu, kuna tafsiri nyingi tofauti juu ya “kuokoka” na hizo tafsiri nyingi si sahihi. Lakini hii hapa chini nadhani ndio tafsiri rahisi zaidi kueleweka.
NINI MAANA YA KUOKOKA?
KUOKOKA ni lugha ya kawaida kabisa, yenye maana ya;
Kunusurika, kusalimika, kupona, kukombolewa, kufunguliwa au kutoka katika janga au hatari fulani.
Mfano:-
- Kunusurika; Paulo aliposafiri mashuani pamoja na watu wengine mia mbili na sabini na sita, alisema;“safari hii itakuwa na madhara na hasara nyingi, si ya shehena na merikebu tu, ila na ya maisha yetu pia … baada ya muda mchache, ukavuma upepo wa nguvu wa namna ya tufani … na kwa maana tulikuwa tukipigwa sana na ile tufani, siku ya pili yake, wakaanza kuitupa shehena baharini. Siku ya tatu wakatupa vyombo vya merikebu kwa mikono yao wenyewe. Jua wala nyota havikuonekana kwa siku nyingi, na tufani kuu ikatushika, basi tukakata tamaa ya kuokoka … na baharia walipotaka kukimbia na kuiacha merikebu … Paulo akawaambia akida na askari, hawa wasipokaa ndani ya merikebu, hamtaweza kuokoka … Shauri la askari lilikuwa kuwauwa wafungwa, mtu asiogelee na kukimbia. Bali akida akitaka kumponya Paulo, akawazuia wasifanye kama walivyokusudia, akawaamuru wale wawezao kuogelea, wajitupe kwanza baharini, wafike nchi kavu … na hivyo watu wote wakapata kuifikilia nchi kavu salama. Tulipokwisha kuokoka, ndipo tulipojua ya kuwa kisiwa kile chaitwa Melita”. (Mdo 27: 1-44. 28:1)
H Hivyo tunaona “KUOKOKA” katika mistari hii, imetumika kama “KUNUSURIKA”.
- Kupona; Wayahudi walimdhihaki Yesu , “Jiponye nafsi yako, ushuke msalabani.
( Mk 15:30)
Sisi je, tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kasha ukadhibitishwa kwetu na wale waliosikia. (Ebr 2:3)
“KUOKOKA” katika mistari hii imetumika kama “KUPONA”.
“Na niseme nini tena? Maana wakati usingetosha kuleta habari za Gideoni, na Baraka, na Samsoni, na Yefta, na Daudi, na Samweli, na za Manabii; Ambao kwa imani, walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba, walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga.
- KUOKOKA katika mistari hii, imetumika kama KUPONA, KUSALIMIKA AU KUNUSURIKA!
- Kusalimika; Wakati Mungu anaangamiza dunia kwa maji ya gharika, Biblia inasema;
“Wala hakuuachilia ulimwengu wa kale, bali alimhifadhi Nuhu mjumbe wa haki na watu
wengine saba, hapo alipoleta gharika juu ya ulimwengu wa wasio mcha Mungu. Tena
akaihikumu miji ya sodoma na Ghomora, akiipindua na kuifanya majivu, akaifanya
akaifanya iwe ishara, kwa watu watakaokuwa hawamchi Mungu baada ya hayo.
Akamwokoa Lutu, yule mwenye haki, aliyehuzunishwa sana na mwenendo wa ufisadi
wa hao wahalifu. (2Pet 2:5-7)
“Hapa KUOKOKA” imetumika kama “KUSALIMIKA” kutoka katika janga la gharika na moto.
- Kufunguliwa au Kukombolewa; Herode alipomtia Petro gerezani ili amuuwe, Biblia inasema;
“Panapo majira yale yale, herode mfalme akanyoosha mikono yake kuwatenda mabaya baadhi ya watu wa kanisa. Akamuuwa Yakobo ndugu yake Yohana kwa upanga. Na akiona yakuwa imewapendeza Wayahudi, akaendelea, akamshika na Petro … akamweka gerezani, akamtia mikononi mwa vikosi vinne vya askari wanne wanne, wamlinde, akitaka baada ya Pasaka, kumtoa na kumweka mbele ya watu. Basi Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa lilikuwa likimwomba Mungu kwa juhudi kwa ajili yake. Hata wakati Herode alipotaka kumtoa, usiku ule ule, Petro alikuwa analala katikati ya askari wawili, alikuwa amefungwa minyororo miwili; walinzi mbele ya mlango wakailinda gereza. Mara malaika wa Bwana akasimama karibu naye, nuru ikamulika mle chumbani, akampiga Petro ubavuni, akamwamsha, akisema, Ondoka upesi! Minyororo yake ikamwanguka mikononi. Malaika akamwambia, jifunge, kavae viatu vyako. Akafanya hivyo. Kisha akamwambia, jivike nguo yako, ukanifuate. Akatoka nje, akamfuata; wala hakujua yakuwa ni kweli, yaliyofanywa na malaika. Bali alidhani kwamba anaona maono. Na walipopita lindo la kwanza na la pili, wakaja hata mlango wa chuma wa kuingilia mjini, ukawafungukia wenyewe. Wakatoka nje, wakapita katika njia moja; mara malaika akamwacha. Hata Petro alipopata fahamu akasema, “sasa nimejua yakini yakuwa, Bwana amempeleka malaika wake na kunitoa katika mkono wa Herode na katika kutazamia kote kwa taifa la Wayahudi”. Na alipokuwa akifikiri hayo, akafika nyumbani kwa Mariamu, mamaye Yohana Marko … na watu wengi walikuwa wamekutana humo wakiomba. Naye alipobisha, kijakazi jina laki Rhoda akaja kusikiliza. Alipoitambua sauti ya Petro, hakufungua mlango, kwa ajili ya furaha, bali alipiga mbio, akaingia ndani, akawaambia kwamba, Petro anasimama mbele ya lango. (Mdo 12:1-14-19)
“KUOKOKA” katika mistari hii, imetumika kama “KUFUNGULIWA” au “KUKOMBOLEWA” katika kifungo.
UHAKIKA WA WOKOVU
Kwahiyo KUOKOKA ni KUNUSURIKA, KUSALIMIKA, KUKOMBOLEWA, KUFUNGULIWA au KUPONA kutoka katika JANGA au HATARI fulani.
Yesu alikuja kuleta wokovu (kuokoa) na Biblia inataja mistari mingi sana juu ya koukoka au wokovu.
Kwa mfano:-
- Yoh 3:16-18; Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanae wa pekee ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyehamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la mwanawe wa pekee.
- Luk 9:59; Kwa maana mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa,
- Yoh 12:47; Na mtu akiyasikia maneno yangu, asiyashike, mimi si mhukumu, maana sikuja niuhukumu ulimwengu, ila niuokoe ulimwengu.
- 1Tim 1:15; Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa ya kwamba, Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi; ambao wa kwanza wao ni mimi.
- 1Tim 2:14; Mungu … hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yalio kweli.
- Efe 2:5,8; Hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo, yaani, mmeokolewa kwa Neema, Kwa maana mmeokolewa kwa Neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;
- 1Kor 1:18; Kwa sababu neno la Msalaba kwao wanaopotea ni upuuzi, bali kwetu tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.
- Mdo 4:10-12; Jueni nyote na watu wote wa Israel ya kuwa, kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye ninyi mlimsulubisha, na Mungu akamfufua katika wafu … kwa jina hilo mtu huyu anasimama ali mzima mbele yenu. Yeye ndiye jiwe lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limekuwa jiwe kuu la pembeni. Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina lingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
Mdo 2:22-24, 36-40, 43-44, 47; Enyi waume wa Israel, sikilizeni maneno haya: Yesu wanazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua; Mtu huyu alipotolewa kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake tangu zamani, ninyi mkamsulubisha kwa mikono ya watu wabaya, mkamwua; ambaye Mungu alimfufua, akifunga uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao…
Basi nyumba yote ya Israel nawajue yakini ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulubisha kuwa Bwana na Kristo. Walipoyasikia hayo wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? Petro akamwambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa watu wote watakao itwa na Bwana Mungu wetu wamjie. Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi …
Kila mtu akaingiwa na hofu; ajabu nyingi na ishara zikafanywa na mitume. Na wote walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote shirika … Wakimsifu Mungu na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.
(Mdo 2:22-24, 36-40, 43-44, 47)
Rum 10:9-10; Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, nakuamini mioyoni mwako yakuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.
Mdo 16:30-31; Kisha akawaleta nje akasema. Bwana zangu, Yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? Wakamwambia, mwamini Bwana Yesu nawe utaokoka pamoja na nyumba yako.
2Kor 6:2; Kwa maana asema, wakati uliokubalika nalikusukia, siku ya wokovu nalikusaidia; Tazama, wakati uliokubalika ndio sasa; Tazama, siku ya wokovu ndio sasa.
Ebr 2:1-3; Kwa hiyo, imetupasa kuangalia zaidi hayo yaliyosikiwa, tusije tukayakosa, kwa maana, ikiwa lile neno lililonenwa na malaika, lilikuwa imara, na kila kosa na uasi, ulipata ujira wa haki. Sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukadhibitika kwetu na wale wanaosikia.
TUMEOKOLEWA KUTOKA KWENYE NINI?
1. TUMEOKOLEWA KUTOKA KATIKA NGUVU YA DHAMBI / UASI
Maana sijui nifanyalo; kwasababu lile nilipendalo silitemdi; Bali lile nilichukialo ndilo nilitendalo … naikiri kuwa ile sheria ni njema. Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. Kwa maana najua kuwa, ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema, kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati … lakini katika viungo vyangu, naona sheria iliyo mbali, inapiga vita na ile sheria ya akili zangu, na kunifanya mateka ya ile sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu. Ole wangu, masikini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti? NAMSHUKURU MUNGU, KWA YESU KRISTO BWANA WETU. (Rum 7:15-15)
“Nanyi mlikuwa wafu kwasababu ya makosa na dhambi zenu. Ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuaata Mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi; ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tama za miili yetu, tulipo yatimiza matendo ya mwili na nia, kukawa kwa tabia yetu watoto wahasira kama na hao wengine. Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; hata wakati ule tulipokuwa wafu kwasababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, mmeokolewa kwa neema akatufufua pamoja naye akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu.”(Efe 2:1-1-2-6)
“Sasa basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti”. (Rum 8:1-2) … “tukijua neno hili, ya kuwa, utu wetu wa kale ulisulubishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike. Tusitumikie dhambi tena … Basi dhambi isitawale ndani ya miili yenu … kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi. Lakini Mungu na ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mli-itii kwa mioyo yenu, ile namna ya elimu (Injili ya wokovu), ambayo mliwekwa chini yake. Na mlipokwisha kuwa huru mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki … kwa maana mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa huru mbali na haki. Ni faida gani mliyopata siku zile kwa mambo hayo mnayo yatahayarikia sasa? Kwa maana mwisho wa mambo hayo ni mauti. Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima. … Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa. (Ezek 28:20-23) … kwa maana mshahara wa dhambi nimauti wa milele, bali karama (zawadi) ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu. (Rum 6:23)
Pia soma; Tito 2:11-12; Tito3:3-4; 2Kor 4:3-4; Efe 4:18-19; 1Tim 1:13-15
TUMEOLOKEWA KUTOKA KATIKA NGUVU ZA GIZA.
“Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa mwana wa pendo lake”. (Kol 1:13)
“Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu, mliwafanya hai pamoja naye, akisha kutusamehe makosa yote; akisha kuifuata ile hati iliyoandikwa kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena akaigongomea msalabani; akiisha kuzivua enzi za mamlaka, na kuzifanya kwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo”. (Kol 2:13-15)
Tazama, nimwewapa amri ya kukanyaga nge na nyoka na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru. (Luk 10:19)
Pia soma; Math 27:45,50-54; Ebr 2:14-15; Luk 11:21-22; Yoh 19:28-30
3. TUMEOKOLEWA KUTOKA KATIKA LAANA YA TORATI.
“Fahamuni basi, yakuwa wale walio na imani, hao ndio wana wa Ibrahim. Na andiko, kwa vile lilivyoona tangu zamani kwamba Mungu atawahesabia haki mataifa kwa imani, lilimhubiri Ibrahim habari njema zamani, kusema, katika wewe mataifa watabarikiwa. Basi hao walio na imani hubarikiwa pamoja na Ibrahim aliyekuwa mwenye imani. Kwa maana wale wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana maana imeandikwa amelaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha Torati, ayafanye. Ni dhahiri ya kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria; kwa sababu mwenye haki ataishi kwa imani. Na torati haikuja kwa imani, bali ,ayatendaye hayo, ataishi katika hayo. Kristo alitukomboa katika laana ya Torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa , amelaaniwa kila mtu aangikwae juu ya msalaba; ili kwamba baraka ya Ibrahim iwafikirie mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya roho kwa njia ya imani”. (Gal 3:7-14, 23-29).
“Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki. (Rum 10:4)
Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki karibu na kutoweka”. (Ebr 8:13)
Basi twaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria …
Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au Sabato; ( Rum 3:28; Kol 2:16)
Pia Mdo 15:1-10-29; Gal 2:16; Rum 8:3; Rum 7:12,14-16; Rum 8:1-4; Yer 31:31-34
4. TUMEOKOLEWA KUTOKA KATIKA DUNIA (UOVU WA DUNIA).
“Neema na iwe kwenu, naamani, zitokazo kwa Mungu Baba, na Bwana wetu Yesu Kristo; ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu, ili atuokoe na dunia hii mbovu, iliyopo sasa. Gal 1:3-4
“Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo. Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmoja wapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie. Na sasa naja kwako; ili wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao. Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umechukia; kwa kuwa wao si waulimwengu, kama mimi nisivyo na ulimwengu. Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; basi uwalinde na yule muovu. Wao sio wa ulimwengu, kama mimi nisivyo waulimwengu. Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndio kweli kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami hivyohivyo naliwatuma hao ulimwenguni. Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli”. Yoh 17:11-19 (14-16)
Pia Yoh 8:21-24 (23); 1Kor 5:9-11; Rum 12:1-2
5. TUMEOKOLEWA KUTOKA KATIKA JEHANUM YA MOTO.
“Kwahiyo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji ikaangamia, lakini mbingu za sasa na nchi, zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na kuangamia kwao wanadamu wasio mcha Mungu. Lakini wapenzi, msilisahau neno hili … Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyodhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu yeyote apotee, bali wote wafikie toba. Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwizi; katika siku hiyo, mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.. Basi kwakuwa vitu hivi vyota vitafumuliwa, hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani? Katika mwenendo mtakatifu na utauwa! Mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo, mbingu zitafumuliwa na zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka. Lakini kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake”. 2 Pet 3:6-13
“Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, nayeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao. Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake;
Na mauti na kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadri ya matendo yake mauti za kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndio mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. Naiwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima alitupwa katika lile ziwa la moto.” Ufu 20:11-15 “Amini, amini nawaambia, yeye asikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna na uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mauti kuingia uzimani”. (Yoh 5:24) Pia Lu 10:20; Fil 4:3; 1Yoh 3:14; Rum 5:6-9;
6. TUMEOKOLEWA KUTOKA KATIKA MAGONJWA.
Nanyi mtamtumikia Bwana Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako na maji yako. Nami nitakuondolea ugonjwa kati yako. (Kut 23:25) … Na Bwana atakuondolea ugonjwa wote, wala hatatia juu yako maradhi yeyote, mabaya uyajuayo …” (Kumb 7:15)
Hata kulipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo, akawatoa pepo kwa jina lake, akawaponya wote waliokuwa hawawezi (wagonjwa). Ili litimie lile neno lililonenwa na Nabii Isaya akisema; “Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu na kuyachukuwa magonjwa yetu.” (Math 8:16-17) “Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote, na udhaifu wa kila aina”. (Math 9:35) “ … Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu; wawatoe na kupoza, magonjwa yote na udhaifu wa kila aina (Math 10:1)
Yeye mwenyewe alizichukuwa dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; Na kwa kupigwa kwake mliponywa (1Pet 2:24) “Hakika ameyachukuwa masikitiko yetu, amejitwika huzuni zetu …. Bali alijeruliwa kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu. Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake; Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. (Isa 53:4 -5)
Damu ya Msalaba iliyoondoa dhambi, ndiyo iliyoondoa magonywa pia. Yatupasa kuyaona magonjwa kama tunavyoiona dhambi. Hatupaswi kuyaona kuwa ni sehemu ya maisha yetu. Magonjwa ni matokeo ya anguko la mwanadamu katika dhambi. Tukiisha okolewa toka dhambini, yatupasa kuokolewa kutoka katika magonjwa pia. Afya njema ni matunda ya msalaba kama ilivyo wokovu.
Tunatakiwa kuchukia magonjwa kama tunavyochukia dhambi, kwasababu yote haya, ni kazi za shetani. Yatupasa kuzikataa na kuzivunja katika maisha yetu. Kifo cha Yesu, kitakuwa hakina maana kamili, kama tutaokolewa katika dhambi, halafu tubaki katika magonjwa pia, wakati Yesu aliyefia dhambi, ndiye aliyefia magonjwa pia. Msalaba ulifanya vyote, uliondoa dhambi na magonjwa pia. “Mwenyewe aliutwa udhaifu wetu na kuyachukuwa magonjwa yetu.” (Math 8:16-17)
7. TUMEOKOLEWA KUTOKA KATIKA UMASKINI
Angalia, utakapokuwa umekula na kushiba, na kujenga nyumba nzuri na kukaa ndani yake. Na fedha yako na dhahabu yako itakapoongezeka. Na kila kitu ulichonacho kitakapoongezeka; Basi hapo moyo wako usiinuke ukamsahau Bwana Mungu wako, aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa … hapo usiseme moyoni mwako, nguvu zangu na uwezo wa mkono wangu, ndio ulionipatia utajiri huo; Bali utamkumbuka Bwana Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri, ili alifanye imara agano lake … (Kumb 8:12-18) Lakini hawatakuwepo masikini kwenu, kwakuwa Bwana atakubariki kweli, katika nchi akupayo Bwana Mungu wako, uimiliki, iwe urithi wako. (Kumb 15:4)
Naye Abrahamu alikuwa tajiri sana kwa mifugo, kwa fedha na kwa dhahabu (Mwa 13:2)
Maana mmejua Neema ya Bwana wetu, Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa masikini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajri. Ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake. (2Kor 8:9) … mkitajirishwa katika vitu vyote, mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu. (2Kor 9:11) … Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu. (Fil 4:19) … Maana yeye yule ni Bwana wa yote, mwenye utajiri kwa wote wamuitao; kwa kuwa, kila atakayeliitia jina la Bwana ataokoka. (Rum 10:12)
Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi, mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi. Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi. (Malaki 3:10 – 12)
Thawabu ya unyenyekevu, ambao ni kumcha Bwana, ni utajiri na heshima, nayo ni uzima.
(Mith 22:4)
Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya dunia; na baraka hizo zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako. Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani, utabarikiwa na uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo. Maongeo ya Ngombe wako, na wadogo wa kondoo zako: utabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga. Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo Bwana atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako watakutokea kwa njia moja; lakini watakimbia mbele kwa njia saba. Bwana ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubariki katika nchi akupayo Bwana wako Mungu wako.
Bwana atakuweka uwe taifa takatifu kwake, kama alivyokuapia; utakapoishika maagizo ya Bwana Mungu wako na kutembea katika njia zako na mataifa yote ya dunia watakuona umeitwa kwa jina la Bwana, nao watakuwa na hofu kwako. Bwana atakufanya uwe na wingi wa uheri, katika uzao wa tumbo lako, na uzao wa wanyama wako, na uzao wa nchi yako, kama Bwana alivyowaapia baba zako kwamba atakupa.
Atakufunulia Bwana hazina yake nzuri, nayo ni Mbingu , kwa kutoa mvua ya nchi yako kwa wakati wake, na kwa kubariki kazi yote ya mkono wako; nawe utakopesha mataifa mengi wala hutokopa wewe. Bwana atakufanya uwe kichwa wala si mkia; nawe utakuwa juu tu, wala huwi chini; utakapo yasikiza maagizo ya Bwana, Mungu wako, nikuagizayo hivi leo,kuyaangalia na kuyafanya; msipokengeuka katika maneno niwaamuruo leo kwa lolote, kwenda mkono wa kuume wala wa kushoto kwa kuifuata miungu mingine na kuitumikia. (Kumb 28:1-14)
Damu ya msalaba iliyoondoa dhambi, ndiyo iliyoondoa umasikini pia, Yatupasa kuuona umasikini kama tunavyoiona dhambi. Umaskini ni matokeo ya anguko la mwanadamu katika dhambi. Tukiisha okolewa katika dhambi, yatupasa kuokolewa katika umasikini pia. Utajiri ni matunda ya msalaba kama ilivyo wokovu. Yatupasa kuchukia umasikini kama tunavyochukia dhambi. Kifo cha Yesu, kitakuwa hakina maana kamili, kama tutaokolewa katika dhambi, halafu tubaki maskini katika mwili pia, wakati Yesu aliyefia dhambi, ndiye aliyefia umasikini pia. Msalaba ulifanya vyote, yaaani uliondoa dhambi na umasikini pia. Biblia inasema; “Maana mmejua Neema ya Bwana wetu, Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa masikini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri. Ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake. (2Kor 8:9) … mkitajirishwa katika vitu vyote, mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu. (2Kor 9:11)
JE UMEOKOKA? UMEOKOLEWA KATIKA HUKUMU IJAYO?
Yesu alikuja kutafuta na kuokoa sisi tuliopotea. Ndio maana alileta wokovu. Kuokoka si dini Fulani au dhehebu Fulani. Kuokoka uzima wa milele ndani ya mtu. “Amini , amini, nawambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka, yuna (ana) uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani”. Ina maana AMEOKOKA kutoka mautini (jehanum). Jehanum ndio mauti ya pili. (Ufu 20:14-15)
Watu wengi wnadhani kutokunywa pombe, kutovuta sigara, kutofanya zinaa, kutoiba, n.k ndio kuokoka na hukumu ya Mungu. Wengi wanadhani, kwenda kanisani, kuimba kwaya, kuhubiri, kuwa mzee wa kanisa au kiongozi wa kikundi, n.k ndio kuokoka na hukumu ya Mungu. Si kweli. Kuna wokovu halisi na matendo au maisha ya wokovu. Watu wengi wanaishi maisha ya wokovu, lakini kwa uhalisi, hawajaokoka bado, hawajampa Yesu mioyo yao na maisha yao.
Kushika sheria za dini na kuishi maisha ya wokovu, siko kunakompendeza Mungu, kama huyo mtu hajampokea Yesu na kumwamini kama Bwana na mwokozi wa maisha yake. Yesu alisema hivi kwa Mungu Baba, “ Na uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma” (Yoh 17:3). Hatuokoki na hukumu ya Mungu kwa kushika sheria, bali kwa kuipokea neema ya wokovu kwa kumwamini Yesu Kristo. “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, ambayo hiyo haitokani na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu (zawadi). Wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu (Efe 2;8-9)
Kushika sheria za dini na kuishi maisha ya wokovu, siko kunakompendeza Mungu, kama huyo mtu hajampokea Yes una kumwamini kama Bwana na mwokozi wa maisha yake. “hali tukijua ya kuwa, mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani ya Kristo Yesu; Sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sheria. Maana kwa matendo ya sheria, hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki” (Gal 2:16; Gal 3:7-14) Kuna wokovu halisi na matendo au maisha ya wokovu. Watu wengi wanaishi maisha ya wokovu, lakini kwa uhalisi, hawajaokoka bado, hawajampa Yesu mioyo yao na maisha yao.
Kuna habari ya mtu wa namna hiyo katika Biblia; aliye shika sheria, aliyedumu katika sala, aliyefunga na kuomba, aliyetoa sadaka nyingi kwa watu maskini, n.k lakini alikuwa hajafanya hatua muhimu kuliko zote ya kumwamini na kumpokea Yesu Kristo, ilia pate uzima wa milele na kuokolewa. Aliitwa Kornelio. Isome katika Matendo ya Mitume 10:1-8, 23-48.
Mungu akamhurumia kuwa, japo amekuwa mwaminifu kushika sheria na kuishi maisha ya kumcha Mungu, lakini kwasababu hajamjua Yesu bado, asingeokoka na hukumu ya milele, kwa maana hana uzima wa milele. Mungu akamtuma malaika kumwambia Kornelio, amfuate Petro, naye atamweleza cha kufanya. Ndipo Petro akaja na akamweleza habari za Yesu, Kornelio na familia yake, wote wakamwamini na kumpokea Yesu. Wakapata wokovu halisi (uzima wa milele). Baada ya hapo, maisha ya wokovu ndipo yanakuwa na maana. Kushika sheria za dini na kuishi maisha ya wokovu, siko kunakompendeza Mungu, kama huyo mtu hajampokea Yesu na kumwamini kama Bwana na mwokozi wa maisha yake. Inawezekana nawe umekuwa mcha Mungu kama Kornelio, lakini hujampokea Yesu moyoni na kumkiri. Mpokee sasa!
NAMNA YA KUPATA WOKOVU (KUOKOKA)
HATUA YA KWANZA; TAMBUA KUWA WEWE NI MWENYE DHAMBI NA UTUBU
DHAMBI ZAKO, KWA KUMAANISHA KUZIACHA.
“Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele” (Rum 3:23). “Tubuni, mkabatizwe kila mmoja kwa jina la Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.” (Mdo 2:38)
HATUA YA PILI; MWANINI NA KUMPOKEA YESU MOYONI MWAKO. TOA
MAISHA YAKO KWAKE, AWE BWANA NA MWOKOZI WAKO.
Yule mlinzi wa gereza akamwambia Paulo na Sila “Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? Wakamwambia, mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako” (Mdo 16:30-31).
“Kwasababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, UTAOKOKA. Kwa maana moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri, hata KUPATA WOKOVU. (Rum 10:9-10)
HATUA YA TATU: ISHI MAISHA YA WOKOVU, MAISHA SAFI YA KUMPENDEZA MUNGU NA KUZISHIKA AMRI ZAKE (NENO LAKE)
“nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi… Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye (Mungu) ikiwa tunashika amri zake. Lakini Yeye asema neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli, katika hili twajua ya kuwa tumo ndani yake….” (1Yoh 2:1-6). Kwahiyo sasa, anza maisha mapya ndani ya Yesu.
“…mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya, ya kale yamepita, tazama! Yamekuwa mapya”. (2Kor 5:17) Jitenge na uovu wote na Usiishi katika maisha ya dhambi tena.
Pia soma Josh 1:8 na Rum 6:1-23.
MAMBO 12 YALIYOKUTOKEA MAISHANI MWAKO BAADA YA KUMPOKEA YESU AWE BWANA NA
MWOKOZI WAKO.
Mpendwa, nataka ujue kwamba, Mungu amefanya mambo mengi makubwa katika maisha yako, tangu saa/siku ile ulipompokea Yesu, kuwa Bwana na Mwokozi na Mwokozi wako. Ni muhimu uelewe kwamba, wewe si yule wa zamani tena. Sahau yaliyopita, kwasababu umefanyika kiumbe kipya. (2 kor 5:17)
Yafuatayo ni baadhi ya mambo yaliyotokea kwako tangu ulipofanya uamuzi huu mzuri na wa busara, wa kumpokea Yesu Kristo, kuwa Bwana wako na Mwokozi wa maisha yako.
KWANZA: UMEFANYIKA MWANA WA MUNGU
Umefanyika mwana wa Mungu, kwasababu umempokea Yesu Kristo na kuliamini Jina lake; Kwasababu Biblia inaema “Bali wote waliompokea, aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake (Yoh 1:12) … Roho (Mtakatifu) mwenyewe, hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu…” (Rum 8:16)
Tangu sasa, wewe ni mmoja wa wana-familia ya Mungu. Nasi tunakukaribisaha kwa upendo wa Kristo. Karibu sana, Baba (Mungu) na sisi tumefurahi kukuona umerudi nyumbani. This is where you belong. We missed you so much. Karibu!
PILI: DHAMBI ZAKO ZOTE ZIMEOSHWA NA KUSAFISHWA KWA DAMU YA YESU NA UMESAMEHEWA KABISA.
Biblia inasema, dhambi zako zote zimeoshwa na kusafishwa kwa damu ya Yesu na umesamehewa zote kabisa, kwasababu umekuja kwa Yesu na umekiri dhambi zako; Kwa maana imeandikwa “katika yeye huyo (Yesu), kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, msamaha wa dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake (Efe 1:17)… Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa nyeupe kama sufu (Isa 1:18)… maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.” (Yer 31:34b) pia soma: Kor 1:14, Ufu 1:5.
TATU: UMEFANYIKA KIUMBE KIPYA
“Hata imekuwa mtu akiwa ndani ya Kristo; amekuwa kiumbe kipya; (mambo ya kale yamepita Tazama! Yamekuwa mapya (2Kor 5:17)… Najua neno moja kuwa, mimi nilikuwa kipofu, na sasa ninaona” (Yoh 9:25)
Kwahiyo sahau maisha yaliyopita, sasa anza maisha mapya ndani ya Yesu.
NNE: ROHO MTAKATIFU ANAISHI NDANI YAKO NA ATAKUWA
PAMOJA NAWE MILELE
“Mkinipenda, mtazishika amri zangu. Nami nitamwomba Baba (Mungu), naye atawapa msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; Ndiye Roho wa kweli, ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwakuwa haumwoni wala haumtambui, Bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu”.
(Yoh 14:15-17) “… Hamjui yakuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu? Na yakuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu alikiharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.” (1Kor 3:16-17)
TANO: UMEHAMISHWA KUTOKA KATIKA NGUVU ZA HETANI au MAMLAKA YA SHETANI au UFALME WA SHETANI, NA KUINGIZWA KATIKA UFALME (MAMLAKA) WA YESU KRISTO.
“Naye (Mungu Baba) alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa mwana wa Pendo lake (Yesu Kristo)” (Kol 1:13)
“Nanyi mfahamu kwamba, mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu, mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa …” (1Pet 1:18)
SITA: UMEHAMISHWA KUTOKA MAUTINI KUINGIA UZIMANI
“Amini amini nawaambia, yeye aliskikiaye neno langu, na kumwamini yeye aliyenipeleka, yuna (ana) uzima wa milele, wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani (Yoh 5:24) “Sisi tunajua yakuwa tumepita kutoka mautini kuingia uzimani…” (1Yoh 3:14). Sasa basi, hakuna hukumu ya adhabu, juu yao walio katika kristo Yesu; kwasababu sheria ya Roho wa uzima, ule ulio katika kristo Yesu, imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti. (Rum 8:1-2)
SABA: UMEOKOLEWA AU UMEOKOKA KUTOKA KATIKA GHADHABU NA ADHABU YA MUNGU.
“Kwa maana, ikiwa Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata ije hukumu. Wala hakuachilia ulimwengu wa kale, bali alimhifadhi (alimwokoa) Nuhu mjumbe wa haki, na watu wengine saba, hapo alipoleta gharika, juu ya ulimwengu wa wasiomcha Mungu. Tena akaihukumu miji ya Sodoma na gomora, akiipindua na kuifanya majivu. Akaifanya iwe ishara kwa wtu watakaokuwa hawamchi Mungu baada ya hayo” (2 Pet 2:4-6)
“Dunia ile ya wakati ule, iligharikishwa kwa maji ikaangamia, lakini mbingu za sasa na nchi, zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilohilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na (siku) ya kuangamia kwao, wanadamu wasiomcha Mungu … Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyodhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu yeyote apotee, bali wote wafikie toba …waokolewe na kupata kujua yaliyo kweli.
((2Pet 3:6-7; 1Tim 2:4)
“Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwizi katika siku hiyo, mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu na vioumbe vya asili vitaunguzwa na kufumuliwa na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea…. mbingu zitfunuliwa, zikiangua na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka. Lakini kama ilivyo ahadi yake, tunatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake. (2Pet 3: 9 -13)
Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki, katika damu yake (Yesu), tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye. (Rum 5:9)
(Kwahiyo)ukimkiri Yesu kwa kinywa chako na kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako yakuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka kwa maana, kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, Na kwa kinywa mtu hukiri, hata kupata wokovu, (Rom 10:9 -10)
Kwa maana mmeokolewa (sio, mtaokolewa) bali; MMEOKOLEWA kwa neema, kwa njia ya imani, ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu, wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisfu. (Efe 2:8)
Maana neema ya Mungu, iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa (Tito 2:11) na itakuwa, kila atakayeliitia jina la Bwana, ataokolewa (Mdo 2:21) …. (Petro) Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya; akisema, jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi (Mdo 2:40)
Walipoyasikia haya, wakachomwa mioyo yao, wakmwambia Petro na mitume wengine; Tutendeje ndugu zetu? Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe, kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu nanyi mtapokea kipawa cha Roho mtakatifu (Mdo 2:37-38). Nao waliopokea neno lake, wakabatizwa. Na siku ile wakaongezeka watu (waume) wapata elfu tatu (41)………Bwana akalizidisha kanisa kila siku, kwa wale waliokuwa wakiokolewa (Mdo 2:47)
NANE: JINA LAKO LIMEANDIKWA KATIKA KITABU CHA UZIMA.
“Lakini msifurahi kwa vile peopo wanavyowatii, bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni (Luk 10:20)…“Na ndani ya mji mtakatifu) hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha mwanakondoo” (Ufu 21:27) …“Na iwapo mtu yeyote, hakuonekan ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto” (Ufu 20:15)…“Naam, nataka na wewe pia, mjoli wa kweli, uwasaidie wanawake hao, maana waliishindania injili, pamoja nami, na wale waliotenda kazi pamoja nami, ambao majina yao yamo katika kitabu cha uzima (Fil 4:3)
TISA: UMEPEWA (UNAZO) NGUVU NA MAMLAKA YOTE JUU YA SHETANI NA NGUVU ZOTE ZA GIZA.
Hata wakati ule tulipokuwa wafu kwasababu ya makosa yetu, alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema. Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika kristo Yesu. (Efe 2:5-6)….. juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina (au cheo) litajwalo (Efe1:21) (akasema)
”Tazama nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui (shetani), wala hakuna kitu kitakachowadhuru (Luk 10:19)… “Nami nitakupa funguo za ufalme wa mbinguni, na lolote utakololifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni, na lolote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni (Math 16:19)… Angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung’oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza, ili kujenga na kupanda (Jer 1:10).
Kila mahali utakapopakanyaga nyayo za miguu yenu, mimewapa ninyi …. hapatakuwa mtu yeyote atakeyeweza kusimama mbele yako, siku zote za maisha yako; kama ulivyokuwa pamoja na Musa, ndivyo nitakanyokuwa pamoja na wewe; sitakupungukia wala sitakuacha (Josh 1:3,5) … Muwe na kiasi na kukesha; kwakuwa mshitaki wenu ibilisi, kama simba aungurumaye, huzunguka zunguka, akitafuta mtu ammeze. Nanyi mpingeni huyo mkiwa thabiti katika imani … (Basi mtiini Mungu. Mpingeni shetani, naye atawakimbia (Yak 4:7) … “Na ishara hizi, zitafuatana na hao waaminio, kwa jina langu watatoa pepo, watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha (kuua), hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya (Mk 16:17-18)
Pia soma: Dan 7:13,14,27; Yer 51:20
KUMI: UNALINDWA KWA ULINZI WA MALAIKA WA MBINGUNI
Malaika wa Bwana hufanya kituo, akiwaangalia wamchao (Mungu) na kuwaokoa
(Zab 34:7) …“Kwakuwa (Mungu) atakuagizia malaika zake, wakulinde katika njia zako zote (Zab 91:11) … Je? hao (Malaika) wote si roho watumikao, wakitumwa kuwuhudumia wale watakaourithi wokovu? (Ebr 1:7,14) Nani (Yohana) nikaanguka mbele ya miguu yake (Malaika) ili nimsujudie; akaniambia, angalia, usifanye hivi, mimi (Malaika) ni nyoli (Mtumishi) wako na w ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudie Mungu…(Ufu 19:10) … Awagusaye ninyi, aigusa mboni ya jicho lake (Mungu). Kwa maana, tazama, nitatikisa mkono wangu juu yao … (Zek 2:8-10). Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu, kwa njia ya imani… (1Pet 1:5)
KUMI NA MOJA: UMEFANYIKA MTUMISHI WA MUNGU.
Watu wengi waliookoka hawajioni au hawajihesabu kuwa ni watumishi wa Mungu. Bali huwaona Wachungaji na Wainjilisti kuwa ndio watumishi wa Mungu. Pengine na wewe unajiona hivyo. Lakini neno la Mungu linasema; Sisi Kanisa (Yaani: Jamii ya waaminio au watu waliookoka), sote kwa pamoja, ni mwili wa Yesu Kristo …
Mungu alipomfufua Yesu Kristo kutoka katika wafu, alimtukuza, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; Juu sana kuliko falme zote na mamlaka zote, “Akavitia vitu vyote chini ya miguu yake. Akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote, kwa ajili ya kanisa, ambalo ndilo mwili wake…” (Efe 1:20-23) “Naye (Yesu) ndiye kichwa cha mwili, yaani cha kanisa….” (Kol 1:18) … Basi ninyi nimekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake… kwa maana katika Roho mmoja, sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu wayahudi, au kwamba tu wayunani; ikiwa tu watumwa, au ikiwa tu huru;
Nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja, kwa maana mwili si kiungo kimoja, bali ni vingi… Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na vioungo vyote vya mwili ule navyo ni vingi, na viungo vyote vya mwili ule navyo ni vingi, ni mwili mmoja, vivyo hivyo na Kristo. (Kor 12,27,13-14,12) … “Basi pana tofauti za karama; Bali Roho ni (mmoja). Tena pana tofauti za huduma, (lakini) Bwana ni mmoja. Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni (mmoja) azitendaye kazi zote katika wote. Lakini Kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kusaidiana. (1kor 12:4-7)
Angalia hili neno “kila mmoja”
“…Mungu amevitia viungo kila Kimoja katika mwili, kama alivyotaka. Lakini kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi? Lakini sasa viungo ni vingi, ila mwili ni mmoja. kila mmoja katika mwili, kama alivyotaka. Lakini kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi? Lakini sasa viungo ni vingi, ila mwili ni mmoja. “(1Kor 12:18-20)
Angalia hilo neno tena “kila kimoja” limejirudia.
“ Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa (kama) apendavyo Roho yeye yule; mwingine (hupewa) imani katika Roho (huyo huyo); na mwingine hupewa kaama za kuponya katika Roho yule mmoja; na mwingine (hupewa) unabii; na mwingine (hupewa) kupambanua roho; na mwingine (hupewa) aina za lugha; na mwingine (hupewa) tafsiri za lugha; Lakini kazi hizi zote, huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake, kama apendavyo yeye. (!Kor 12:8-11)
Angalia hilo neno “kila mmoja” limejirudia tena
Kwa hiyo, kama vile katika mwili, kila kiungo kina kazi yake (ya kujenga mwili); Vivyo hivyo, katika mwili wa Kristo, yaani Kanisa, kila muumini, ana kazi yake ana huduma yake, na karama yake na wajibu wake, katika kujenga mwili wa Kristo. Wewe na mimi, tu watumishi wa Mungu. Jione hivyo na ujihesabu hivyo. Mungu anataka utumie karama na uwezo aliokupa, ili kuuvunja ufalme wa shetani, na kujenga ufalme wa Kristo duniani. Neno la Bwana likamjia, kusema, kabla sijakuumba katika tumbo, nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; Nimekuweka kuwa nabii wa Mataifa. Ndipo niliposema, Aah! Bwana Mungu! Tazama, siwezi kusema; maana mimi ni mtoto lakini Bwana akaniambia, usiseme mimi ni mtoto; … usiogope kwasababu ya hao, maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoe, asema. Bwana.
Ndipo Bwana, akanyoosha mkono wake, akanigusa kinywa changu; Bwana akaniambia; Tazamani, nimetia maneno yangu kinywani mwako; Angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung’oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; Ili kujenga na kupanda (Yer 1:4 -10) “… enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi (wangu) mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu; Na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. (Math 28:18-20).
KUMI NA MBILI: UMEPEWA AHADI KUBWA MNO NA ZA THAMANI NA MUNGU
Tangu umeingia katika familia ya wana wa Mungu umepewa urithi wa baraka za Mungu. Umeingizwa katika mkondo wa baraka na ahadi kubwa na nyingi mno katika kriso Yesu.
“Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana (wa Mungu), Mungu alimtuma Roho wa mwanawe mioyoni mwetu, aliaye Aba, yaani Baba. Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena, bali u mwana (wa Mungu); Na kama u mwana, basi u mrithi kwa Mungu” (Gal 4:6-7)
“Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu…, ili kwamba, Baraka ya Ibrahimu, iwafikie mataifa ktika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya roho kwa njia imani … Na kama ninyi ni wa kristo, basi mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawa sawa na ahadi” (Gal 3:13-14,29).
“Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa Baraka zote za rohoni, katika ulimwengu waro ho, ndani yake Kristo. (Efe 1:3)… Tena kwa hayo, ametukirimia ahadi kubwa mno za thamani, ili kwamba, kwa hizo (ahadi na baraka) mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani, kwa sababu ya tamaa.”(2Pet 1:4) Kwa mfano:-
Ahadi ya Baraka – Kumb 28:1 – 14; Law 26:1-13
Ahadi ya mafanikio – Zab 1:1 -3; Josh 1:8-9
Ahadi ya utajiri – Kumb 15:14; 2Kor 8:9 / 2Kor 9:8,11
Ahadi ya Afya njema – Kut 15:26: Kumb 7:15
Ahadi ya Ulinzi – Zab 91:11; Zab 121:1-8
Ahadi ya Akili nzuri – Zab 119:97-100; Zab 111:10
Ahadi ya Wokovu kwa familia - Mdo 16:31; Isa 54:13 – 14
UHAKIKA WA WOKOVU.
Sasa elewa vizuri kuwa, TAYARI UMEOKOLEWA, hapa hapa duniani, na si baada ya kufa. Kwasababu Biblia inasema, “Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa (ni) hukumu”
(Ebr 9:27). Mungu ametuletea wokovu hapa hapa duniani, ili tuupokee hapa hapa duniani. Baada ya kufa, hakuna wokovu tena, bali hukumu. Mtu anayesubiri wokovu baada ya kufa, atakuwa amechelewa!
Kumbuka habari ambayo Yesu alisema “Palikuwa na mtu mmoja tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula siku zote kwa anasa. Na alikuwepo masikini mmoja, jina lake Lazaro, aliyewekwa mlangoni pa tajiri, na ana vidonda vingi. Naye masikini alitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri, hata mbwa wakalamba vidonda vyake”.
Hii ina maana kwamba, tajiri hakuwa mcha Mungu; Kwa maana hakumjali masikini, pamoja na kwamba alikuwa na uwezo. Masikini alikuwa na hali mbaya sana, ya njaa na ugonjwa, hata hakuweza tena kuwafukuza mbwa waliomkaribia. Ndio maana, Tajiri alipokufa, alikwenda motoni. “ikawa yule masikini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu”. (Hii ina maana, masikini alikuwa mcha Mungu). “Yule tajiri naye akafa, akazikwa. Basi kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali na Lazaro kifuani mwake. Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwasababu ninateswa katika moto huu. Ibrahimu akasema, mwanangu, kumbuka ya kwamba, wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa. Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi, kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu, wasivuke kuja huku.
(Tajiri) akasema, basi, Baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu (duniani), kwakuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso. Ibrahimu akasema, (kule duniani) wanao Musa na Manabii; na wawasikilize wao. (Tajiri) akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu. (Ibrahimu) akamwambia, wasipowasikia Musa na Manabii (wahubiri mbalimbali), hawatashawishiwa, hata mtu akifufuka katika wafu”.
BAADA YA KUFA NI HUKUMU! HAKUNA WOKOVU! Mungu ametuletea wokovu hapa hapa duniani, ili tuupokee hapa hapa duniani, kabla ya kifo kutujia. Baada ya kufa, hakuna wokovu tena, bali hukumu. Mtu anayesubiri wokovu baada ya kufa, atakuwa amechelewa, kama yule Tajiri!
Ni muhimu pia uelewe kwamba, tajiri hakwenda motoni kwa sababu alikuwa tajiri; wala masikini hakusalimika au hakuokoka kwasababu alikuwamasikini. Utajiri si dhambi, wala umasikini si utakatifu. Uhusiano wako na Mungu ndicho kitu kitakachoamua utakwenda kuishi wapi milele. Wala si fedha yako, wala elimu yako, wal dini yako! Kitu pelee kitakachoamua wapi utaishi milele, ni uhusiano wako na Mungu. “Basi tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote NA HUO UTAKATIFU (ucha Mungu) ambao hapana mtu atakayemwona Mungu, asipokuwa nao” (Ebr 12:14)
Unaweza ukaupata ulimwengu wote, ukawa na kila kitu duniani; utajiri, elimu nzuri, dini nzuri, kazi nzuri, nyumba nzuri, mshahara mzuri, magari mazuri, viwanda hata migodi ya thamani. Lakini kama huna wokovu, yaani uhusiano mzuri na Mungu, hutaweza kuingia mbinguni. “Kwani itamsaidia nini mtu, akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake?” (Math 16:26) Hakuna faida!
Utajiri halisi ni ule wa ndani (wokovu) ukiunganishwa na wanje (mali na pesa). Ndio maana Yesu anasema “Nayajua matendo yako, yakuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi kwasababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu. Kwakuwa wasema, mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe ni mnyonge, na mwenye mashaka, na masikini, na kipofu, na uchi.” (Ufu 3:15-17).
Kumbe unaweza ukavaa na kupendeza mbele za watu, na kumbe mbele za Mungu uko uchi kabisa! Unaweza ukawa mbabe na mjanja mbele za watu, na kumbe mbele za Mungu ukawa mnyonge na si kitu kabisa! Unaweza kudhani unaona kwa macho, na kumbe umefichwa vitu vingi halisi, huvioni! Unaweza ukawa tajiri wa mali za ulimwengu, na kumbe mbele za Mungu ukawa masikini kabisa, kwasababu huna ule utajiri halisi, yaani wokovu. Yesu anamalizia kwa kusema “Nakupa ushauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto (yaani WOKOVU), UPATE KUWA TAJIRI, na mavazi upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.”
Dhahabu inayotajwa hapo ni WOKOVU, kama ilivyoandikwa katika Mathayo 13:44-46; “Tena Ufalme wa mbinguni umefanana na HAZINA iliyositirika katika shamba, ambayo mtu aliopoiona, aliificha; na kwa furaha yake, akaenda akauza vyote alivyo navyo, akalinunua lile shamba. Tena Ufalme wa mbinguni umefanana na mfanya biashara, mwenye kutafuta LULU NZURI; naye alipoona LULU MOJA YA THAMANI KUBWA, alikwenda akauza vyote alivyo navyo, akainunua”. Hapa, tunaambiwa habari za wokovu kuwa ni KITO cha thamani! Wokovu ni LULU! Wokovu ni DHAHABU Ya thamani nyingi! Wokovu ni HAZINA njema!
Maadam umempokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wako, Mungu anakwambia “unao uzima wa milele” sasa hivi ukiwa hapa hapa duniani. “Amini amini nawaambia, yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka, YUNA (ANAO) UZIMA WA MILELE; WALA HAINGII HUKUMUNI, BALI AMEPITA KUTOKA MAUTINI KUINGIA UZIMANi” (Yoh 5:24). Mungu anakwambia “unao uzima wa milele” sasa hivi ukiwa hapa hapa duniani. Sio kwamba “utakuwa nao” bali ansema “unao” yaani sasa! Na tena anasema, kwa kuwa unao uzima moyoni mwako, hutaingia hukumuni, bali “umepita” kutoka mautini kuingia uzimani! Sio “utapita”, bali Mungu anasema, “tayari umepita” kutoka mautini, kuingia uzimani.
Pia imeandikwa hivyo katika 1Yoh 3:14. Na tena 2Wakorintho 6:2 inasema; “… Tazama, wakati uliokubalika ndio sasa; TAZAMA, SIKU YA WOKOVU NDIO SASA.
Baada ya kufa, hakuna wokovu tena, bali hukumu. Mtu anayesubiri wokovu baada ya kufa,atakuwa amechelewa!
UWE NA UHAKIKA WA WOKOVU WAKO. JUA KWAMBA, KWA NEEMA YA MUNGU, UMEOKOKA! Kwa maana imeandikwa “MMEOKOLEWA KWA NEEMA, KWA NJIA YA IMANI; HIYO HAIKUTOKANA NA NAFSI ZENU, NI KIPAWA CHA MUNGU”. (Efe 2:8)
KANUNI ZA MAISHA YA KILA SIKU YA KIKRISTO.
(KANUNI ZA MAISHA YA WOKOVU)
Mpendwa, inabidi ufahamu kwamba, kuokoka haimaanishi tayari umefika mbinguni; Bali inamaana kwamba; ndio tu umeanza safari salama ya kwenda mbinguni. Mtu ambaye hajaokoka, ni kwamba hajaanza kabisa safari ya kwenda mbinguni. Na unafahamu kwamba, wakati mwingine, si wasafiri wote humaliza safari zao; Kwasababu katika safari huwa kuna vikwazo mbalimbali. Wengine huishia mwanzoni kabisa mwa safari, wengine huishia katikati ya safari na wengine huishia mlangoni kabisa na kushindwa kuimaliza safari.
Safari ya mbinguni pia, ina vikwazo vingi. Ndio maana Biblia inasema “mlango ni mwembamba na njia imesonga, iendayo uzimani” (Math 7:14). Ni shauku ya Mungu na yetu pia, kwamba uimalize salama safari yako ya kwenda mbinguni, ambayo uliianza siku uliyompa Yesu Kristo maisha yako na kuokoka. Si njia rahisi. Kuna mambo mengi ya kukukwaza na kukuzuia. Lakini Mungu amekuahidi ushindi katika mambo yote hata kukufikisha mbinguni salama.
Biblia inasema; “Hata (Mitume) walipokwisha kuihubiri injili katika mji ule, na kupata wanafunzi wengi, wakarejea mpaka Listra na Ikonio na Antiokia, wakifanya imara roho za wanafunzi, na kuwaonya wakae katika ile imani, na yakwamba imetupasa kuingia katika Ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi” (Mdo 14:21-22). Yesu alisema; “Ulimwenguni mnayo dhiki, lakini jipeni moyo, mimi (Yesu) nimeushinda ulimwengu” (Yoh 16:33). Lakini “Katika mambo yote tunashinda na zaidi ya kushinda, katika yeye (Yesu) aliyetupenda” (Rum 8:37). Hebu sema kama Paulo “Nayaweza mambo yote, katika yeye (Mungu) anitiaye nguvu” (Fil 4:13)
Ebr 11:32-38 inasema “Na niseme nini tena? Maana wakati usingetosha kuleta habari za Gideoni, na Baraka, na Samsoni, na Yefta, na Daudi, na Samweli, na za Manabii; Ambao kwa imani, walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba, walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga, walitiwa nguvu baada ya kuwa wadhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya wageni. Wanawake walipokea wafu wao, waliofufuliwa. Lakini wengine waliumizwa vibaya hata kuuwawa … wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam kwa mafungo na kwa kutiwa gerezani. Walipigwa kwa mawe, walikatwa kwa misumeno, walijaribiwa, waliuwawa kwa upanga, walizunguka-zunguka wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; … wakiteswa, wakitendwa mabaya; … Walikuwa wakizunguka-zunguka katika nyika na katika milima, na katika mapango na mashimo ya nchi.”
Haiwezekani hawa mashujaa wa imani, washinde vita na upinzani huo, na kuingia mbinguni kwa ushindi, kwa nguvu zao wenyewe. Ni lazima kuna siri fulani iliwasaidia kumaliza safari yao kwa ushindi. Siri hizo na kanuni hizo ndizo zilizowasaidia wengi na ndizo zinazotusaidia wengi, kuishi maisha ya wokovu kwa ushindi.
Mpendwa, fahamu kwamba, NEEMA YA WOKOVU ambayo umepewa na Yesu, ni ya thamani kuu kuliko kitu chochote duniani. Hakuna fedha wala dhahabu inayoweza kununua wokovu. Wala hakuna kitu chochote duniani kinachoweza kulingana na wokovu ambao Yesu ametupa. Si fedha, wala dhahabu, wala almasi, wala elimu, wala cheo, wala pesa au chochote kinachoweza kulingana na zawadi ya wokovu tulionao katika Yesu. Wokovu ulionao sasa, ndicho kitu cha gharama zaidi na cha thamani zaidi kuliko vitu vyote duniani.
Kila kitu cha gharama kama vile redio, televisheni, friji, gari, compyuta, n.k. hutengenezwa na kuuzwa pamoja na kitabu chenye maelezo ya jinsi ya kukitumia (manual book), kinachokuwezesha kukitumia hicho kifaa au chombo, kwa usahihi bila kukiharibu. Kama mmiliki wa kifaa au chombo hicho hatafuata maelekezo ya watengenezaji wa chombo kile, basi kifaa hicho kitaharibika na kushindwa kulitimiza kusudi lake.
Vivyo hivyo, na WOKOVU huu tuliopewa na Bwana Yesu, ni wa thamani na gharama kubwa, tena unaweza kuharibika kirahisi (very fragile). Hivyo, unatakiwa kuutunza kwa umakini na uangalifu mkubwa, kwa kufuata maelekezo, kanuni na siri za maisha ya wokovu. Siri hizo na kanuni hizo, ndizo zilizowasaidia wengi na ndizo zinazotusaidia wengi, kuishi maisha ya wokovu kwa ushindi, bila kuharibu. Bwana Yesu mtoa uzima, na aliye mwanzilishi wa wokovu wetu, ametupa kitabu cha maelekezo (manual book) cha namna ya kuutunza wokovu wetu, ili tusiuharibu, tusiuchafue wala kuupoteza. Kitabu hiki kinaitwa BIBLIA TAKATIFU!
Kila siku hakikisha unasoma maelekezo ya kutosha kwa ajili ya wokovu wako. Na kwa kuyafuata maagizo ya NENO LA MUNGU, hautaweza kamwe kuuharibu, kuuchafua au kuupoteza wokovu, yaani uhusiano mzuri na Mungu. Nawe utaweza kuimaliza safari yako ya mbinguni kwa salama na uhahika, kama wale mashujaa wa imani. Angalia maandiko yanavyosema; “Kitabu hiki cha torati (Neno la Mungu) kisiondoke kinywani mwako; bali uyatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawa sawa na maneno yake yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana”. (Joshua 1:8)
KANUNI ZA MAISHA YA USHINDI
1. DUMU KATIKA MAOMBI – ONGEA NA MUNGU KILA SIKU
KWA SALA NA MAOMBI.
“Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba, huku na shukurani …” (Kol 4:2) “… imewapasa kumwomba Mungu siku zote, wala msikate tamaa” (Luk 18:1) … “Kwa sala zote na maombi, mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote”
(Efe 6:18) … “Furahini siku zote; ombeni bila kukoma; shukuruni kwa kila jambo, maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika kristo Yesu.” (1Thes 5:16-18)
Kwanini Biblia inasisitiza sana tudumu katika maombi? Maombi ni namna ya wewe kuwasiliana na Mungu Baba. Tangu umeokoka, umefanyika mwana wa Mungu. Maongezi huunganisha familia. Maongezi huimarisha uhusiano. Ili uzidi kukua katika kumjua Mungu na uhusiano wako na Mungu uweze kuimarika, yakupasa kudumu sana katika maombi na sala. Tamani kujifunza kuomba, tena tamani kiwango chako cha maombi kiongezeke. “Ikawa (Yesu) alipokuwa mahali fulani akiomba, alipomaliza, mmoja katika wanafunzi wake akamwambia, Bwana, tufundishe sisi kusali, kama vile Yohana alivyowafundisha wanafunzi wake” (Luk 11:1).
Katika maombi kuna faida nyingi;-
Kwa mfano:
(i) Katika maombi unapata kumjua Mungu na kuwa karibu nae zaidi.
ii) Katika maombi unapata uongozi wa Mungu na kujua mapenzi ya Mungu
(iii) Katika maombi unapata nguvu za kushinda dhambi na majaribu.
(iv) Katika maombi anapata nguvu za kumpinga shetani na kuvunja kazi zake.
(v) Katika maombi unapata kumweleza Mungu mahitaji yako na haja zako.
(vi) Katika maombi unapata kukua katika karama, huduma na vipawa.
(vii) Katika maombi unapata amani na kujaa furaha ya Roho Mtakatifu.
(viii) Katika kuomba unapata baraka na kibali cha Mungu (favour) maishani .
Ndio maana Neno la Mungu linasisitiza kudumu katika maombi. Tenga muda wa kuomba kila siku. Na uwe mwaminifu. Utaona furaha, amani, Baraka, Ushindi na Mafanikio katika maisha yako na kazi zako.
Uwe na muda wako binafsi, wa kufanya maombi. Biblia inasema, Yesu alituonyesha mfano; “Walikwenda kila mtu nyumbani kwake; naye Yesu akaenda mpaka mlima wa Mizeituni (kuomba) (Yoh 8:1) … Hata alfajiri na mapema sana, akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko. (Mk 1:35) Naye alipokwisha kuwaaga makutano, alipanda mlimani faraghani, kwenda kuomba. (Math 14:22-23) … Yeye (Yesu) siku hizo za mwili wake, alimtolea (Mungu) maombi na dua na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu. (Ebr 5:7)
2. SOMA BIBLIA – MRUHUSU MUNGU ASEME NAWE KILA SIKU KWA NENO LAKE.
“Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana”
(Kol 3:16) …” kila andiko lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema” (2Tim 3:16-17) … “kama watoto wachanga waliozaliwa sasa, yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu”. Kitabu hiki cha torati (Neno la Mungu) kisiondoke kinywani mwako; bali uyatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawa sawa na maneno yake yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana”. (Joshua 1:8) Neno la Mungu li hai lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga ukatao kuwili…” Ebr 4:12-13, Pia soma Ebr 5:12-13.
3. KUSANYIKA / JUMUIKA NA WAAMINIO WENGINE, KUMWABUDU MUNGU
NA KUJIFNZA NENO LA MUNGU.
“Bwana akalizidisha kanisa kila siku, kwa wale waliokuwa wakiokolewa … na watu walioamini, walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote shirika … na siku zote kwa moyo mmoja, walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha, na kwa moyo mweupe, wakimsifu Mungu na kuwapendeza watu wote … wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali. (Mdo 2:42-47) … Tena nawaambia, ya kwamba, wawili wenu watakapo patana duniani katika jambo lolote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu; nami nipo papo hapo katikati yao (Math 18:19-20). Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana (Kol 3:16)
Pia soma 2Tim 2:22; Heb 5:12-13.
4. ISHI MAISHA MASAFI NA MATAKATIFU, YANAYO MPENDEZA MUNGU
“Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? Hasha! Sisi tulioifia dhambi, tutaishije tena katika dhambi? … Tukijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale, ulisulubishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilika, tusitumikie dhambi tena; … Vivyo hivyo, ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu wa dhambi, na walio hai kwa Mungu, katika Kristo Yesu … Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zenu; wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi; Bali jitoeni wenyewe kwa Mungu, kama walio hai baada ya kufa, na (vitoeni) viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki. Kwa maana dhambi haita watawala ninyi, kwasababu hamuwi chini ya sheria, Bali chini ya Neema.
… Lakini Mungu na shukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile maana ya elimu (wokovu) ambayo mliwekwa chini yake; na mlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki … kwakuwa kama mlivyovitoa viungo vyenu vitumiwe na uchafu na uasi mpate kuasi, vivyo hivyo sasa, vitoeni viungo vyenu vitumiwe na haki mpate kutakaswa.
Kwa maana mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa huru mbali na haki. Ni faida gani basi mliyoipata siku zile kwa mambo hayo mnayoyatahayarikia sasa? Kwa maana mwisho wa mambo hayo ni mauti. Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele. Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; Bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu, Bwana wetu. (Rum 6:1-2, 6, 11-14, 17-23)
Basi nasema neno hili, tena nashuhudia katika Bwana, tangu sasa msienende kama mataifa waenendavyo, katika ubatili wa nia zao; ambao akili zao zimetiwa giza, nao wamefarakanishwa na uzima wa Mungu, kwasababu ya ujinga uliomo ndani yao, kwasababu ya ugumu wa mioyo yao; ambao wakiisha kufa ganzi, wanajitia katika mambo ya ufisadi (uchafu), wapate kufanyiza kila namna ya uchafu kwa kutamani. Bali ninyi, sivyo mlivyojifunza Kristo; ikiwa mlimsikia mkafundishwa katika yeye, kama kweli ilivyo katika Yesu, mfue kwa habari ya mwenendo wa kwanza, utu wa zamani, unao haribika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya. Na mfanye wapya katika roho ya nia zenu, mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli (Efe 4:17-24)
“Iliyobaki ndugu, tunawasihi na kuwaonya kwamba, mwenende katika Bwana Yesu; kama mlivyopokea kwetu jinsi iwapasavyo kuenenda na kumpendeza Mungu, kama nanyi mnavyoenenda, vivyo hivyo mpate kuzidi sana. Kwakuwa mnajua ni maagizo gani tuliyowapa kwa Bwana Yesu. Maan hayo ndiyo mapenzi ya Mungu, (ndiyo) kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; Kila mmoja wenu, ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; si katika hali ya tamaa mbaya, kama mataifa wasiomjua Mungu. (1Thes 4:1-5) … “Jitengeni na ubaya wa kila namna” (1Thes 5:22), “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na (pia tafuteni kwa bidii kuwa na) huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana, asipokuwa nao.” (Ebr 12:14) …“Bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, mtakuwa watakatiku, kwa kuwa mimi ni mtakatifu” (1Pet 1:15-16)
5. UWE SHAHIDI WA YESU KWA WATU WENGINE.
“Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu” (1Kor 4:1) … Kwa urahisi kabisa, mwambie mtu mwingine, mambo ambayo Mungu amekutendea, ya kwamba Mungu ameyabadilisha maisha yako. Waambie kwamba, ulikuwa na maisha maovu na kwamba Yesu amekusamehe, amekuokoa na amekupa maisha mapya, ambayo ndiyo maisha ya uzima milele. Kisha waambie kuwa, Yesu anawapenda, na anataka kuingi katika maisha yao. Waulize kama wako tayari kumpokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yao. Kama wako tayari, waombee wapokee wokovu kama wewe; Nawe utakuwa mtumishi wa Mungu kwa kuifanya kazi ya Mungu.
Wewe ni mtumishi wa Mungu (1Kor 4:1) Yesu anakwambia “Enenda zako, nyumbani kwako, na kwa watu wa kwenu, kawahubiri ni mambo gani makuu aliyokutendea Bwana, na jinsi alivyokurehemu. Akaenda zake, akaanza kuhubiri katika Dekapoli, ni mambo gani makuu, Yesu aliyomtendea; watu wakastaajabu”. (Marko 5:19)
NAMNA YA KUSHUHUDIA INJILI KWA WATU WENGINE.
Waeleweshe kwamba;
WANADAMU WOTE TUMEFANYA DHAMBI.
“… (wanadamu) wote tumefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu” (Rum 3:23)
ADHABU YA MUNGU INAUJIA ULIMWENGU WOTE.
“…mbingu na nchi zimewekwa akiba kwa moto, zikilindwa hata siku ya hukumu, na kuangamia kwao wanadamu wasio mcha Mungu” (2Pet 3:7)
HAKUNA MWANADAMU ANAYEWEZA KUJIOKOA MWENYEWE.
“ni nani awezaye kuokoka? Yesu akawakazia macho akawaambia, kwa wanadamu, hilo haliwezekani; Bali kwa Mungu, yote yanawezekana” (Math 19:25-26)
IKO NJIA MUNGU AMEANDAA, YA KUOKOKA KATIKA ADHABU HIYO.
YESU NDIYE NJIA YA KUOKOKA NA HUKUMU YA MUNGU.
“ Yesu akamwambia, Mimi ndimi Njia, na Kweli, na Uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya Mimi” (Yoh 14:6) “Aniaminiye Mimi , anao uzima … haingii hukumuni, bali amepita kutoka hukumuni kuingia uzimani” (Yoh 5:24) Ukimkiri na kumwamini ……utaokoka”
(Rum 10;9-10)
MUULIZE KAMA YUKO TAYARI KUMWAMINI NA KUMPOKEA YESU.
MWONGOZE SALA YA TOBA NA KUPOKEA WOKOVU. (Mdo 8:35-39)
Kwa mfano;
Ee Bwana Yesu, ninakuja kwako. Ninakiri mimi mwenye dhambi na makosa mengi. Nazijutia dhambi zangu na kutubu kweli. Ninaomba unisamehe na kuniosha kwa damu yako ya thamani. Ninaomba uniokoe maisha yangu. Nafungua moyo wangu na ninakukaribisha. Ingia ndani yangu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Uwe Bwana na Mwokozi wangu tangu sasa. Weka ndani yangu, uzima wa milele na uhakika wa wokovu. Asante Yesu kwa kuniokoa. Naomba unipe nguvu za Roho wako Mtakatifu, nianze maisha mapya, nisirudi nyuma tena. Katika jina la lako takatifu, Yesu Kristo, ninaomba na kushukuru, Amen.
WEWE NI MSHINDI.
Mpendwa, nataka kukwambia, tunaishi katika ulimwengu mbaya na mchafu sana. Lakini katikati yake, kuna watu walioipata furaha na amani ya kweli, ambayo ni bora na ya thamani mno kuliko vitu vyote. Watu hawa wanadharauliwa na kutukanwa, wengine wanateswa na kunyanyaswa, lakini wao hawajali. Wanachukiwa na ulimwengu wote lakini siku zote , wamejaa furaha na amani ya Mungu. Ni mabwana wa nafsi zao, wameushinda ulimwengu na hakuna kinachoweza kuwazuia. Wanaonekana wako katika upande wa washindi tu.
Watu hawa wanaitwa WAKRISTO. WAMEOKOKA, WAMEJAZWA NA ROHO MTAKATIFU na WANAKWENDA MBINGUNI. Nataka ujue kwamba, MIMI PIA MMOJA WAO! Na kwasababu NA WEWE UMETUBU DHAMBI ZAKO NA KUMPOKEA YESU KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO, WEWE PIA NI MMOJA WETU. NASI TUNAKUKARIBISHA KATIKA FAMILIA YA MUNGU, KWA UPENDO MKUBWA.
YESU ANAKWAMBIA; “…USIOGOPE WALA USIFADHAIKE, KWA KUWA BWANA MUNGU WAKO YUKO PAMOKA NAWE KILA UENDAKO … SITAKUACHA WALA SITAKUPUNGUKIA ….NIKO PAMOJA NAWE HATA MWISHO WA DUNIA …. UWE MWAMIIFU HATA KUFA, NAMI NITAKUPA TAJI YA UZIMA.
(Joshua 1:9,5 Math 28:20 Uu 2:10)
“Kwasababu hiyo, tangu (sisi) tulipopata habari za imani yenu katika Bwana Yesu, na pendo lenu kwa watatakatifu wote, hatuachi utoa shukrani (kwa Mungu) kwa ajili yenu na tukiwakumbuka katika sala zetu, ili Mungu wa Bwana Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima naya ufunuo katka kumjua yeye; macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la wito wake jinsi lilivyo, na utajiri wa utukufu wa urithi wake kwa watakatifu jinsi ulivyo; na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio jinsi, kwa kadri ya utendaji wa nguvu za uweza wake ….” (Efe 1:15-19),
“Desciples of Christ” tunakuombea sana. Ni kwasababu tunakupenda na tunakujali. Ni maombi yetu kwa Mungu Baba kwamba, uweze kukuwa katika neema ya wokovu na katika kumjua sana Yesu Kristo Bwana na kuimaliza safari yako salama ya kwenda mbinguni. Nasi tunaamini kabisa ya kuwa “Yeye (Mungu) aliyeanzisha kazi njema mioyoni mwenu, ataimaliza (ataikamilisha) hata siku ya Kristo Yesu.” (Fil 1:6)