Wednesday, May 11, 2011

Gwajima

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ametoa mpya kwa kutahadharisha kuhusu tiba ya kikombe cha Mchungaji Ambilikile Masapile wa Samunge, Loliondo kwa kusema kuwa endapo dawa hiyo anayoitoa inaponyesha watu asibughudhiwe wala asipigwe vita.
Gwajima alitoa tahadhari hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita kanisani kwake jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Tanganyika Pakers, Kawe alipokuwa akihojiwa na mwandishi wa gazeti hili juu ya msimamo wake juu tiba anayoyatoa mchungaji Masapile maarufu kwa jina la Babu.
Alisema kwamba hajajua kama dawa hiyo inaponyesha watu au laa na kueleza kuwa, kama wagonjwa wanaoitumia wanapona ni jambo zuri, hivyo hakuna sababu ya kubughudhiwa bali apewe ushirikiano ili aendelee kuwasaidia wagonjwa.
“Hao watu wanaompiga vita Masapile ina maana wameshindwa kuwasaidia wagonjwa na ndiyo maana wanakimbiwa na kubakia kulalamika huku wakiponda huduma anayoitoa mchungaji huyo. Wagonjwa ni wajanja sana, wanaangalia ni wapi wanaweza kupata uponyaji,” alisema Gwajima.
Aliongeza kusema kuwa, kunywa dawa ya miti si dhambi kwani hata vidonge vinavyotumika kutibu magonjwa mbalimbali vinatokana na mimea isipokuwa huwa vinatengenezwa kiwandani, hivyo haoni tatizo kwa Masapile kutumia uponyaji wa mizizi anayodai kuoteshwa na Mungu.

No comments: