watoto wanafanya ni kitanda |
jamani na kamari pia? |
watoto wanafanya ni kitanda |
jamani na kamari pia? |
Monday, 23 May 2011 21:58 |
Tausi Ally MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, jana iliwahukumu kifungo cha miaka mitano jela kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rajabu Maranda na binamu yake, Farijala Hussein baada ya kupatikana na hatia kwenye mashtaka sita kati ya manane ya kujipatia fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA). Mbali ya kifungo hicho, pia wametakiwa kurudisha Sh1.8 bilioni walizochota kwenye akaunti hiyo katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na endapo watashindwa kufanya hivyo, mali zao zitakamatwa na kufilisiwa. Hukumu hiyo iliyochukua zaidi ya saa mbili, ilisomwa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Ilvin Mgeta kwa niaba ya jopo la mahakimu watatu waliokuwa wakiisikiliza. Mahakimu wengine ni Focus Bampikya na Saul Kinemela. Maranda na mwenzake walikuwa wanakabiliwa na mashtaka manane yakiwamo ya kula njama, kughushi, wizi, kuwasilisha hati za uongo na kujipatia ingizo la fedha kwa njia ya udanganyifu kwenye akaunti kiasi cha Sh1.8 bilioni, mali ya BoT wakijaribu kuonyesha kuwa Kampuni yao ya Kiloloma & Brothers imepewa idhini ya kukusanya deni la Kampuni ya BC Cars Export ya Mumbai, India. Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mgeta alisema katika shtaka la pili la kughushi hati za usajili wa kampuni, Farijala atatumikia kifungo cha miaka mitatu jela, katika shtaka la tatu la kughushi hati ya makubaliano, Maranda na Farijala wote watatumikia kifungo cha miaka mitano jela.Alisema katika shtaka la nne ambalo nalo pia ni la kughushi, wote watatumikia kifungo cha miaka mitano jela. Katika shtaka la tano la kuwasilisha nyaraka za kughushi BoT, Maranda atatumikia kifungo cha miaka miwili jela. Katika shtaka la sita, Hakimu Mgeta alisema wote watatumikia kifungo cha miaka mitatu jela na kwenye shtaka la nane la kujipatia ingizo kwa njia ya udanganyifu kila mshtakiwa atatumikia kifungo cha miaka mitatu jela. Hakimu Mgeta Baada ya kumaliza kusoma hukumu hiyo, Hakimu Mgeta alifafanua kuwa vifungo vyote vitakwenda sambamba, hivyo kila mshtakiwa atatumikia kifungo cha miaka mitano jela.Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Hakimu Mgeta kwa niaba ya jopo hilo alisema wote wana kesi ya kujibu kwenye shtaka la pili, tatu, nne, tano, sita na la nane.Alisema katika shtaka la kwanza ambalo ni la kula njama ya kutenda kosa la wizi na la saba la wizi, yamefutwa kwa sababu mahakama imewaona hawana hatia baada ya mashahidi tisa wa upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha kama ni kweli walifanya makosa hayo. Baada ya mahakama kuwatia hatiani, Wakili Mkuu wa Serikali, Boniface Stanslaus aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa washtakiwa hao kwa kuzingatia kiasi cha fedha walizochukua na madhara yaliyowafika wananchi hasa ikizingatiwa kwamba hiyo ni kesi ya kwanza ya EPA kutolewa hukumu. “Naomba mahakama itumie mamlaka yake chini ya kifungu cha Sheria cha 358 (1) cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), kutoa amri kuwa washtakiwa hawa warudishe hela kwa mwenyewe ambaye ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Stanlaus wakati akiwasilisha maombi yake mahakamani hapo. Wakili Magafu Hata hivyo, Wakili wa Maranda, Majura Magafu alipinga hoja hiyo na kusema kuwa makosa yanayowakabili wateja wake hayapo chini ya kifungu hicho cha sheria, hivyo hawapaswi kurejesha fedha hizo. “Waheshimiwa kifungu cha 358 cha Kanuni ya Uendeshaji wa Kesi za Jinai iliyorekebishwa mwaka 2009, makosa ambayo yanamtaka mtu anayedaiwa kurudisha fedha zinazodaiwa kuibwa ni yale yaliyopo kwenye sura ya 27 na 32 ya Kanuni ya Adhabu," alisema Wakili Magafu. Magafu alisema makosa wanayowakabili wateja wake kwa mujibu wa Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 61 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2009, ni ya kughushi na kwamba yapo kwenye sura ya 36 ambayo adhabu yake inasomwa kwenye sura ya 37 ya Kanuni ya Adhabu. Alisema kosa la kujipatia ingizo kwa njia ya udanganyifu lipo chini ya kifungu cha sheria cha 305 na kwamba inapatikana kwenye sura ya 31 ya Kanuni ya Adhabu, hivyo kutokana na hali hiyo, aliomba ombi la upande wa mashtaka la kutaka wateja wake waamuliwe kurejesha fedha zinazodaiwa kuibwa lisiangaliwe na mahakama kwa sababu halisemwi katika vifungu vilivyotajwa kisheria. Wakati Magafu akiendelea kutoa hoja zake, Wakili Stanslaus aliingilia kati na kusema kuwa wao waliomba washtakiwa hao waamuliwe kulipa fedha hizo wanazodaiwa kuziiba chini ya kifungu cha sheria cha 358 (1) kwa sababu washtakiwa hao pia wanakabiliwa na shtaka la kujipatia ingizo kwa njia ya udanganyifu. Akiendelea kuwasilisha hoja zake, Magafu alisema kuwa: "Ni rai yetu tunaomba washtakiwa wasipewe amri iliyoombwa ya kutaka warejeshe hizo fedha na kwamba kama serikali itaona wana haja ya kurudisha hizo fedha kuna njia mwafaka wanayotakiwa kufuata wapate fedha hizo." Aliiomba mahakama iwaonee huruma kwa sababu hayo ni makosa yao ya kwanza, hawajawahi kutiwa hatiani katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwamba wanategemewa na familia zao zenye watu wengi. ‘Waheshimiwa kama mlivyoona, hati ya makubaliano iliyopelekwa BoT ambao walithibitisha kuwapo kwa mawasiliano na hatimaye walitoa fedha hiyo inayoonyesha kuna watu walitumika kuwapotosha washtakiwa," alisema Magafu. Aliongeza kuwa Maranda na Hussein ni wagonjwa wanaosumbuliwa na ugonjwa wa figo hivyo kutokana na hali hiyo, aliiomba mahakama kwa mamlaka iliyopewa, chini ya kifungu cha 138 cha Kanuni ya Adhabu, pamoja na kuwatia hatiani washtakiwa bado inaweza kuwaachia huru kulingana na mazingira.Aliiomba mahakama wakati inapotoa adhabu iangalie kifungu hicho cha sheria. Kutolewa hukumu Baada ya kutolewa kwa hoja hizo, ilipotimia saa 6:00 mchana, Hakimu Mgeta aliwasimamisha washtakiwa na kuwaeleza kuwa Jopo la Mahakimu limesikiliza hoja zilizotolewa na wakili wao, Magafu na limezizingatia na kuziheshimu lakini kulingana na uzito wa kesi: “Tumepima pamoja tumefikia uamuzi wa kutoa adhabu yenye kuonya, watatumikia kifungo cha miaka mitano jela, kuhusu kurudisha fedha zilizochukuliwa tumesikiliza hoja za Magafu, lakini tunatofautiana naye, hivyo washtakiwa wote wanatakiwa kurejesha kiasi hicho cha fedha na wasipofanya hivyo, mali zao zitakamatwa na kufilisiwa,” alisema Mgeta. Hakimu huyo alisema kama upande wa utetezi haukuridhika na hukumu hiyo, haki ya kukata rufaa ipo wazi. Mara baada ya kumaliza kutolewa kwa hukumu hiyo, washtakiwa walipelekwa gereza la Ukonga kuanza kutumikia vifungo vyao. Washtakiwa kutakata rufaa? Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya hukumu hiyo, Wakili Magafu alisema wateja wake hawajaridhika na hukumu hiyo, hivyo wataomba mwenendo mzima wa kesi hiyo ikiwamo hukumu ili waisome halafu watajua cha kufanya. Awali, hukumu hiyo ilipangwa kutolewa Aprili 29, mwaka huu lakini iliahirishwa. Hukumu hiyo ilitolewa baada ya Magafu kufunga ushahidi wao mara baada ya washtakiwa hao wawili kumaliza kutoa utetezi. Akifunga ushahidi wa utetezi, Magafu alidai kuwa wanaamini mahakama imewasikiliza mashahidi tisa wa upande wa mashtaka na wateja wake kwa umakini hivyo wanaiachia itoe uamuzi wake. Baada ya Magafu kutoa maelezo hayo, Wakili Stanslaus alisema kuwa hata wao (Serikali) wanaiachia mahakama itoe uamuzi. Awali, Machi 23, mwaka 2009 Stanslaus ambaye alikuwa akisaidiana na Wakili wa Serikali, Timon Vitalis walifunga ushahidi huo mara baada ya shahidi wa tisa, Steven Mwakalukwa (54), ambaye ni Mkaguzi wa Mahesabu ya Ndani katikaBoT, kumaliza kutoa ushahidi wake. Mbali ya kesi hiyo iliyomalizika jana, Maranda anakabiliwa na kesi nyingine nne za aina hiyo katika mahakama hiyo wakati Farijala anakabiliwa na kesi tatu pia za aina hiyo ambazo zitaendelea kusikilizwa wakati wakiendelea kutumikia kifungo vyao. |
He died this morning at his Magomeni home.
Kwa mujibu wa mwanawe aitwaye Hassan, Sheikh yahya amefariki kutokana na heart failure. Aliamka asubuhi ya leo akiwa buheri wa afya, akaanza kazi yake ya kuona wenye matatizo wanaokuja kwake.
Kama kwenye saa tatu hivi, akaanza kujisikia vibaya, akapewa glasi ya juisi lakini hali haikutulia. wakaamua kumkimbiza katika hospitali moja maeneo ya Morocco na alipofikishwa hapo madaktari wakasema tayari ameshafariki dunia.
Mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwake na atazikwa kesho jijini Dar.
Ameimaliza safari yake. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina
|
||
|
||
Mwanamke huyo kwa sasa amelazwa katika hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam, majeruhi mwingine amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Chanzo cha vurugu hizo hakijawekwa bayana kwa kuwa wanajeshi wanadai kuwa wananchi ndiyo walioanza kupanga mipango ya kuwavamia askari waliokuwa doria eneo hilo la machimbo ambalo wananchi wamepigwa marufuku wasiendele na uchimbaji. Lakini wananchi wamekanusha madai ya askari hao na kudai kuwa, wanajeshi waliwavamia kwenye makazi yao baada ya kuzozana na baadhi ya wachimbaji ambao walikuwa wanachimba kokoto eneo ambalo si la jeshi. Tukio hilo lilitokea Jumapili saa nne asubuhi Kunduchi wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam. Katika eneo hilo la machimbo ya kokoto kwa sasa baadhi ya watu wameligeuza makazi yao, lakini pia eneo hilo liko liko karibu na Kambi ya JWTZ Kunduchi. Kwa muda mrefu kumekuwa na mvutano kati ya wachimbaji na wanajeshi kuhusu uchimbaji wa kokoto unaofanywa eneo hilo. Uchimbaji kwa kutumia baruti ulikatazwa na jeshi na kuwataka wananchi wafanye shughuli zao nje ya mita 500 kutoka kambi ya JWTZ. Mmoja wa majeruhi, John Kadengu aliliambia gazeti hili kuwa wakati tukio hilo linatokea, alikuwa nyumbani kwake mara akavamiwa na kundi la wanajeshi na ndipo akashitukia anapigwa kirungu begani na baadaye akapigwa ngwala na kuanguka chini. “Mimi nimeumia na hivi natoka hospitali Muhimbili wameniambia kuwa bega langu limeteguka,” alisema Kadengu aliyedai wanajeshi waliwatesa kwa kuwarusha kichura kwenye matope na pia kuwaamuru wapande kilima huku wakiruka kichura. Alidai kuwa, wakati anaruka kichura kwa vile alishapigwa, alijisikia vibaya akawaomba wanajeshi wampumzishe; lakini wakaendelea kumtaka aruke kichura na baadaye hali yake ikawa mbaya akakimbizwa kwenye zahanati ya kijeshi kabla ya kupelekwa Muhimbili. Diwani wa Kata ya Kunduchi, Janet Rithe alisema, yeye alipigiwa simu wakati tafrani hiyo inaanza na alipoenda eneo la tukio alishuhudia wanajeshi wakivamia makazi ya wananchi na kuwapiga virugu na mikanda hali iliyomfanya akimbilie kambini ili kutoa taarifa kwa mkuu wa kambi. “Nilishuhudia kwa macho yangu wakiingia kwenye nyumba moja iliyoko eneo hilo la machimbo wakampiga mwanamke mjamzito ambaye baadaye tulimkimbiza Hospitali ya Mwanyamala; lakini bahati mbaya ile mimba imetoka,” alisema Janet. Alidai alipofika kambini alipokewa kwa lugha za kejeli kutoka kwa wanajeshi waliokuwa getini. “Waliniambia usilete siasa hapa au wewe ndio unaowatuma watu wako waje kutufanyia fujo,” alidai diwani huyo. Alisema, alikuta watu 32 wanashikiliwa na baada ya kuruhusiwa kuonana na mkuu wa kambi, aliwasihi wawaachie wananchi waliokuwa wanashikiliwa ili zifanywe taratibu za kuwashitaki kiraia. Alisema baada ya kuwaachia na kupelekwa ofisi ya kata ndipo walipowakimbiza watu wanne ambao walijeruhiwa vibaya hospitalini ambako wawili wameruhusiwa kutoka; lakini wengine wawili akiwemo mama huyo mjamzito bado wamelazwa. Ofisa Habari wa JWTZ, Meja Joseph Masanja alikanusha wanajeshi kuwapiga raia na akasisitiza kuwa, walioumia ni waliojaribu kukimbia kwa hofu baada ya kuwaona wanajeshi wakienda eneo hilo. Akielezea tukio hilo kwa kina, Masanja alisema, wananchi waliokutwa katika eneo hilo hawakuumizwa wala kupigwa na askari wao. Alisema siku hiyo, wanajeshi waliokuwa doria katika eneo hilo waliwakamata baadhi ya watu wakiwa wanachimba kokoto. Alisema wakati wakiwahoji, walijitokeza kundi la wananchi ambao waliwaambia wanajeshi hao kuwa hawawezi kuliachia eneo hilo. Alisema wananchi hao huku wakiwa wamebeba silaha waliwazingira askari hao wawili waliokuwa doria tayari kuwazuru wanajeshi hao.“Baada ya kuona hivyo wale wanajeshi hawakuwa na namna ya kufanya hivyo wakaomba msaada kwa wenzao waliokuwa kambini.” Masanja alisema, kundi hilo la wanajeshi walipofika eneo hilo walitumia mbinu za kijeshi za kuwaokoa wenzao; hivyo wananchi baada ya kuliona kundi hilo walikimbia ovyo na wengine wakaumia. Alisema, baadhi ya wananchi walikamatwa na kupelekwa kambini na wakati huo tayari viongozi wa wananchi hao akiwemo diwani walikuwa tayari wameshafika kambini hapo kwa ajili ya kufanya mazungumzo na viongozi wa kambi. “Uongozi wa kambi ulifanya mashauriano na diwani na kuamriwa kuwa wahusika waliokamatwa wapelekwe kwenye vyombo vya sheria kupitia ofisi za serikali za mitaa,” alisema Meja Masanja. Alisema wananchi hao walikamatwa na vifaa vya kuchimbia kokoto pamoja na malori mawili . Alisema eneo hilo ni la jeshi kwani liko ndani ya mita 500 kutoka kambi ya jeshi. |