Monday, May 9, 2011

Obama: bin Laden alisaidiwa Pakistan


Rais Obama ametoa wito kwa serikali ya Pakistan kuchunguza mtandao ambao ulimpa hifadhi Osama bin Laden kwenye nyumba ya siri, ambako aliuliwa juma lilopita na makamando wa Marekani.
Rais Obama wa Marekani
Akihojiwa kwenye televisheni, Bwana Obama alisema hana ushahidi kuonesha kuwa watu ndani ya serikali ya Pakistan wakimsaidia bin Laden, lakini ni jambo ambalo linafaa kuchunguzwa.
Lakini alisema, lazima kulikuwa na watu wakimsaidia na inafaa kuchunguzwa.
Pakistan imekanusha tuhuma kuwa, kusudi, ilimpa hifadhi kiongozi wa Al Qaeda, na imetoa amri kufanywe uchunguzi, kwanini idara yake ya ujasusi ilishindwa kumpata.

No comments: